Wadau Ireland tunapenda kuchukua nafasi hii kuwakumbuka kina mama wakati wa siku yao 'Mothers Day' iliyosherehekewa duniani tarehe 22.03.09. Kwa kunukuu maneno ya mzee mmoja (wa kale) kuwa maisha ya kina Mama ni sawa na Pilot anaye-endesha ndege. Kina mama pia ni pilots katika familia. Pilot huhakikisha kuwa ndege inasafiri salama hata anapokuwa amechoka au kujisikia kusinzia. Kina mama katika familia huhahakikisha watoto wanaongozwa vema siku hadi siku bila kuchoka.
Mama ni mwalimu katika familia. Mtoto kama mwanafunzi atamuuliza mama swali hata kama anajua mama hatokuwa na jibu; ataomba kila kitu hata kama anajua mama hatakuwa na uwezo. Je, ni nani hakuwahi kulia akiwa mdogo? Je, ulipolia ulimtaja nani? Mama! Mwenyezi mungu awape kina mama wote duniani afya njema ya kuwawezesha kuishi maisha marefu na hata kuweza kuonja matunda ya watoto wao. Kina Mama wa Afrika, kwa namna ya pekee, mnahitaji pongezi kubwa; mungu awabariki. Kina mama vijijini Afrika mzigo wenu kimaisha unatia huruma kubwa. Siku ya kina mama duniani itoa changamoto kwa viongozi wote Afrika kuinua maisha ya kinamama vijijini.
WALIMU NI NGUZO YA MAENDELEO-MAJALIWA
-
*WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa walimu ni nguzo kuu ya maendeleo
ya taifa lolote hapa duniani kwani ndio wanaotoa rasilimaliwatu yenye elimu
am...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment