Sunday, March 29, 2009

Kiswahili miaka ya 80 na 90.

Hapo zamani za kale!
Mdau mmoja katuandikia kwa vituko kutukumbusha miaka ya 80 na 90 wakati kiswahili kilipokuwa kinafanyiwa 'make up'. Wakati huku ulaya, na hasa uingereza, wanaikumbuka the 80s & 90s kwa kutamba kwa boybands; Tanzania tunaikumbuka mi80 na mi90 kwa mabadiliko makubwa ya kiswahili. Sisi wa mikoani tulisubiria kwa hamu misamiati iliyokuwa ikitokea miji mikubwa kama vile Dar, Arusha, Zoo na Iringa. Mi80 na mi90 huko mikoani ilipambwa kwa misamiati mbalimbali, ambayopia iliweza kutuchanganya kitafsiri. Mfano
  • Tukitoe, Tukinyanyue= (mara- kitoe king'ombe kidogo)
  • Chalii= kijana (Ar, kijana; mza- kulala chali)
  • Mshikaji = rafiki (bila mabadiliko)
  • Buzi = (Mara, mbuzi mkubwa; Dar- mtu anayekunyonya kifedha)
  • Mambo fresh= Mara, neno fresh lilitumiwa na wauza maziwa kumaanisha ubora wa bidhaa hiyo.
  • Kihiyo= (Dar na Arusha, mtu aliyetuhumiwa kwa kuiba kwa kutumia kalamu; Msm, neno kihiyo lilimaanisha-kichaa!
Manano kama haya yalitesa sana mikoani, vijana walioshindwa kuyatumia katika maongezi walionekana wa-shamba! Lakini pia tusisahau export za mikoani zilizowahi kutoa changamoto miji mikubwa. Export maarufu za kimisamiati toka mikoani ambazo pia zilitafsiriwa kimakosa ni kama ifuatavyo:
  • Mura= (Dar, tafsriri=dume)- Mara, tafsiri= Shujaa
  • Msimbe= Dar, bibi/girlfriend)- mara, mke au binti mwenye kutembea na mtu aliyeolewa.
  • Ndege - Arusha, neno hili lilimaanisha nuksi; mza- neno ndege lilimaanisha uharibifu wa zao la mpunga kwa ndege wengi!
  • Magiro ganu- (msm, watu hawa= Dar-?)
  • Nyang'au - msm & mza= mvamizi, Pwani = nyama kavu
  • Kereng'ende = Bara (msm, mza na Shy = mtu wa kawaida, Dar, moro = mtu baki
  • Bumunda- Msm (mza & msm mtu asiyejiweza kimasomo)
  • Piga Ng'ombe - (kanda ya ziwa = kaba kabali kwa nia  ya kunyang'anya/kwapua= Dar, Pwani, Moro, Iringa = piga ng'ombe kwa fimbo.
  • Kusomesha = (Dar- chombeza, msm, mza & Ar = kijana kumshawishi binti)
Je misamiati gani inayokukumbusha mi80 & mi90?

No comments:

Post a Comment