Ndugu Watanzania Ireland
Tunapenda kutangaza kuundwa kwa kamati ya chama cha watanzania hapa Ireland. Kwa taratibu za uongozi si vema kwa Mwenyekiti na Katibu kufanya uamuzi wa kila jambo bila kuwa na chombo saidizi ndani ya umoja wetu. Dhumuni mojawapo la kupendekeza kuundwa kwa kamati ya chama ni kutuwezesha kuwa na mchango wenye uwiano mkubwa katika kutoa mawazo, majadiliano na kufikia uamuzi wa mambo mbali mbali yanayotuhusu.
Kamati ya chama ikiundwa na uwiano mzuri weye wawakilishi toka vitongoji mbalimbali hapa Ireland itasaidia kupanga taratibu mbalimbali zitakazoweza kuendesha umoja na hivyo kupunguza idadi ya mikutano ya mara kwa mara (isiyo ya lazima).
Tunapenda kukuza umoja huu, Tanzania Ireland kama tawi la watanzania waishio nje ya nchi bado ni changa. Mabibi na Mabwana tunaomba mjitokeze ili tusonge mbele!
Tunaomba yeyote mwenye kupenda kujiunga na 'Kamati ya chama' atume jina lake kwenye barua pepe:swahili@live.ie
WALIMU NI NGUZO YA MAENDELEO-MAJALIWA
-
*WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa walimu ni nguzo kuu ya maendeleo
ya taifa lolote hapa duniani kwani ndio wanaotoa rasilimaliwatu yenye elimu
am...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment