Sunday, March 29, 2009

Kiswahili miaka ya 80 na 90.

Hapo zamani za kale!
Mdau mmoja katuandikia kwa vituko kutukumbusha miaka ya 80 na 90 wakati kiswahili kilipokuwa kinafanyiwa 'make up'. Wakati huku ulaya, na hasa uingereza, wanaikumbuka the 80s & 90s kwa kutamba kwa boybands; Tanzania tunaikumbuka mi80 na mi90 kwa mabadiliko makubwa ya kiswahili. Sisi wa mikoani tulisubiria kwa hamu misamiati iliyokuwa ikitokea miji mikubwa kama vile Dar, Arusha, Zoo na Iringa. Mi80 na mi90 huko mikoani ilipambwa kwa misamiati mbalimbali, ambayopia iliweza kutuchanganya kitafsiri. Mfano
  • Tukitoe, Tukinyanyue= (mara- kitoe king'ombe kidogo)
  • Chalii= kijana (Ar, kijana; mza- kulala chali)
  • Mshikaji = rafiki (bila mabadiliko)
  • Buzi = (Mara, mbuzi mkubwa; Dar- mtu anayekunyonya kifedha)
  • Mambo fresh= Mara, neno fresh lilitumiwa na wauza maziwa kumaanisha ubora wa bidhaa hiyo.
  • Kihiyo= (Dar na Arusha, mtu aliyetuhumiwa kwa kuiba kwa kutumia kalamu; Msm, neno kihiyo lilimaanisha-kichaa!
Manano kama haya yalitesa sana mikoani, vijana walioshindwa kuyatumia katika maongezi walionekana wa-shamba! Lakini pia tusisahau export za mikoani zilizowahi kutoa changamoto miji mikubwa. Export maarufu za kimisamiati toka mikoani ambazo pia zilitafsiriwa kimakosa ni kama ifuatavyo:
  • Mura= (Dar, tafsriri=dume)- Mara, tafsiri= Shujaa
  • Msimbe= Dar, bibi/girlfriend)- mara, mke au binti mwenye kutembea na mtu aliyeolewa.
  • Ndege - Arusha, neno hili lilimaanisha nuksi; mza- neno ndege lilimaanisha uharibifu wa zao la mpunga kwa ndege wengi!
  • Magiro ganu- (msm, watu hawa= Dar-?)
  • Nyang'au - msm & mza= mvamizi, Pwani = nyama kavu
  • Kereng'ende = Bara (msm, mza na Shy = mtu wa kawaida, Dar, moro = mtu baki
  • Bumunda- Msm (mza & msm mtu asiyejiweza kimasomo)
  • Piga Ng'ombe - (kanda ya ziwa = kaba kabali kwa nia  ya kunyang'anya/kwapua= Dar, Pwani, Moro, Iringa = piga ng'ombe kwa fimbo.
  • Kusomesha = (Dar- chombeza, msm, mza & Ar = kijana kumshawishi binti)
Je misamiati gani inayokukumbusha mi80 & mi90?

Kampuni za kusafirisha mizigo kwenda Tanzania

Wazalendo!
Kwa yeyote anayejua kampuni zinazosafirisha mizigo kwenda TZ tokea hapa Ireland, tunaomba maelezo. Kuna watu wengi wanahitaji kusafirisha mizigo kwenda TZ (kwa unafuu) lakini hawajui jinsi gani. Tasaidiane!

Monday, March 23, 2009

Special Thanks to all Mothers around the world

Wadau Ireland tunapenda kuchukua nafasi hii kuwakumbuka kina mama wakati wa siku yao 'Mothers Day' iliyosherehekewa duniani tarehe 22.03.09. Kwa kunukuu maneno ya mzee mmoja (wa kale) kuwa maisha ya kina Mama ni sawa na Pilot anaye-endesha ndege. Kina mama pia ni pilots katika familia. Pilot huhakikisha kuwa ndege inasafiri salama hata anapokuwa amechoka au kujisikia kusinzia. Kina mama katika familia huhahakikisha watoto wanaongozwa vema siku hadi siku bila kuchoka.
Mama ni mwalimu katika familia. Mtoto kama mwanafunzi atamuuliza mama swali hata kama anajua mama hatokuwa na jibu; ataomba kila kitu hata kama anajua mama hatakuwa na uwezo. Je, ni nani hakuwahi kulia akiwa mdogo? Je, ulipolia ulimtaja nani? Mama! Mwenyezi mungu awape kina mama wote duniani afya njema ya kuwawezesha kuishi maisha marefu na hata kuweza kuonja matunda ya watoto wao. Kina Mama wa Afrika, kwa namna ya pekee, mnahitaji pongezi kubwa; mungu awabariki. Kina mama vijijini Afrika mzigo wenu kimaisha unatia huruma kubwa. Siku ya kina mama duniani itoa changamoto kwa viongozi wote Afrika kuinua maisha ya kinamama vijijini.

Sunday, March 22, 2009

KAPELO ZA KIMOBITELI

JAMANI  SUMMER INAKUJA ZIANDAENI SIMU ZENU KWA KUNUNUA KOFIA ZA VIMOBITELI. NA ZENYEWE PIA ZINA FEELING.

WADAU TUSAIDIANE KATIKA MKWAJA HUU (Recesion)

WADAU NINAWAZO KAMA KUNA MTU ANAHITAJI KITU AU MWINGINE ANA KITU CHA ZIADA UNAWEZA KUWEKA HUMU ILI ANEYEHITAJI AWEZE KUSAVE PESA.
PIA TUNAWEZA KUBADILISHANA VITU HUMU.

Tuesday, March 17, 2009

St. Patrick's Festival 17.03.09

Wadau hawa walipopewa mwaliko wa kuhudhuria St. Pat's Festival, Ireland, walikumbuka kubeba myamvuli; Ati waliambiwa Ireland kuna mvua nyinigi na hali ya hewa hubadilika mara kwa mara. Miye niliwanasa kwenye Kamera, Katika shangaa shangaa yangu kwenye Parade hapo O'Connell St. mida ya saa saba. Baada ya kutafakari picha hii nikagundua kuwa myamuli hii ilikuwa imeandaliwa kupambana na jua kali lililotwanga mtaa mzima wa O'Connell na kusababisha Mto Lifey kunyauka! O'Connell st. imeshuhudia Global Warming- evidence tazama Picha. Wadau tuleteeni picha mlizopiga leo kwenya Festival hii- baadhi ya picha zangu zimeungua tokana na jua kali!!

Monday, March 16, 2009

Kuundwa kwa Kamati ya chama: Tanzania Ireland

Ndugu Watanzania Ireland
Tunapenda kutangaza kuundwa kwa kamati ya chama cha watanzania hapa Ireland. Kwa taratibu za uongozi si vema kwa Mwenyekiti na Katibu kufanya uamuzi wa kila jambo bila kuwa na chombo saidizi ndani ya umoja wetu. Dhumuni mojawapo la kupendekeza kuundwa kwa kamati ya chama ni kutuwezesha kuwa na mchango wenye uwiano mkubwa katika kutoa mawazo, majadiliano na kufikia uamuzi wa mambo mbali mbali yanayotuhusu.
Kamati ya chama ikiundwa na uwiano mzuri weye wawakilishi toka vitongoji mbalimbali hapa Ireland itasaidia kupanga taratibu mbalimbali zitakazoweza kuendesha umoja na hivyo kupunguza idadi ya mikutano ya mara kwa mara (isiyo ya lazima).
Tunapenda kukuza umoja huu, Tanzania Ireland kama tawi la watanzania waishio nje ya nchi bado ni changa. Mabibi na Mabwana tunaomba mjitokeze ili tusonge mbele!

Tunaomba yeyote mwenye kupenda kujiunga na 'Kamati ya chama' atume jina lake kwenye barua pepe:swahili@live.ie

Canon Multipass C70 Fax,Printer,Copier- BURE

Ndugu mdau
Tunashukuru kwa kuchukua uamuzi wa kugawa Printer- Bure. Kwa moyo wako mkunjufu, toa maelezo unapatikana wapi-Anwani yako, ili wanaohitaji waje kuchukua. Ajabu!uliweza kupata muda wa ku-'scan' picha ya printer na kutoa 'spec' zake lakini hukupata muda wa kueleza vizuri unapatikana wapi, anwani, tel # etc.

Friday, March 13, 2009

Canon Multipass C70 Fax,Printer,Copier- BURE




Habari Wadau, Ninazo hizo CANON MULTIPASS C-70 zilizotumika , kwa anayetaka tuwasiliane kwa email hii (azania@eircom.net). Nitagawa mwisho 2 kwa mtu, Pia uweze kuja kuchukua mwenyewe sina nafasi ya kudeliva. Nyingi zinafanya kazi ila sina uhakika kuwa zote zitafanya kazi. Specs zake hizo hapo chini. Asanteni

Canon MultiPASS C70 All-In-One InkJet Printer
Consumer Rating:

Information:
The MultiPASS C70 is a highly featured, full color, all-in-one PC connectable multifunctional printer. The small and compact unit offers Small Office/Home Office users the ability to color fax, color.
The MultiPASS C70 is a highly featured, full color, all-in-one PC connectable multifunctional printer. The small and compact unit offers Small Office/Home Office users the ability to color fax, color print, color copy, color scan and also to PC fax. The MultiPASS C70 is the perfect all-in-one color desktop solution.??The MultiPASS offers superb quality color bubble jet printing to give all output that professional look. The MultiPASS C70 takes advantage of a 'no fuss' cartridge replacement system, ensuring full printer functionality with ease. If the majority of the output is color, a color cartridge is used, however, if the output is predominantly text then the cartridge can be quickly and easily swapped with no mess, for a black cartridge. The MultiPASS C70 allows printing on to many types of media; plain paper, high resolution paper, glossy photo paper, T-shirt transfers to name but a few, ensuring users can get maximum creativity and capability from one compact unit.


MDAU.

Tuesday, March 10, 2009

40+ Years still depending on aid from the West.

For decades, Africa has remained a continent of aid recipient (simply beggers)! African leaders have failed to come up with strategies that can liberate the continent economically. I mean failed due to the fact that the continent has for so long been used to receiving easy cash to support struggling buggets. African countries have been used to others doing things for them. This includes the hearty charities of western countries, the generous rock stars working day and night to raise cash to combat hunger in sub-sahara and many more. The contintent has continued begging from the very countries it claimed independence from. Of all aid recipients, Africa is the biggest economic recepient. One wonders why it has not been possible for Africa to shine economically and stop receiving aid year on year from the west. We, Africans, were led to believe that colonialism cemented long term ties to an extent that it left the continent poorer and poorer. On the other hand, others have argued that following independence dictatorship by few leaders led to massive migration of skilled people to Western countries hence contributing to building western economies.
These are just excuses. Why is it that a small country like Ireland (wih 4millions), which was colonised for three hundred years, has managed to build its economy and reached a point of supporting a vast African continent of almost billions of people?
We have begged from the West and now decide to extend to East. We have now shifted to Asia. The Chinise are increasingly interested in the piece of the pie in Africa. The increased influence of China in Africa means another extension to the already existing aid inflow to Africa. China will help any Cuntry that suits its own agenda-energy and minerals. To sight a few examples; the construction of Railways in  Zambia; construction of highways in Ghana; redevelopment of Nigeria rail Network; Construction of National Stadium in Tanzania and in Ghana; construction of oil product facilities in Khartoum etc.
We need revolution in the continent, I don't mean war but different thinking, different ways of doing things. My grandfather used to say 'ukimwonesha mtoto kuvua samaki hata omba mboga kwa jirani'. We have abundant resources but why can't we learn to fish ourselves? Why do we need to ask the Chinese? We blamed the West for their tricky contracts on various projects in Africa, how can we be sure that the chinese and Indians won't do what the west have done.
by Mr. M Jogoo

Monday, March 2, 2009

YOPET

Sisi YOPET (Youth Organization for Poverty Reduction - Tanzania), tumesaka kwa Muda mrefu ushirikiano wa watanzania wenzetu waishio Ireland na viunga vyake. sisi sio Njo, ni kikundi chenye watu takriban 420 members sasa. Makao yetu makuu ni hapa hapa Kunduch-Dar es Salaam, Tanzania. tumejifunga kutafuta mpenyo wa kuondokana na Umaskini iwapo tutawezeshwa. tuna malengo yetu na mikakati. iwapo tutapata mawasiliano yenu mazuri, na moyo wenu wa uzalendo tutashirikiana kujikwamua.

Pastor Bihagaze
Mwenyekiti

SHUKRANI

UONGOZI TANZANIA IRELAND, WADAU IRELAND, UNAPENDA KUTOA SHUKRANI KUFUATIA ZIARA YA WAZIRI MKUU, MIZENGO P. PINDA TAREHE 25 HAD 27 FEB 09. NI MATUAMAINI YETU KUWA KUSHIRIKI KWENU KWENYE MAANDALIZI, MAPOKEZI NA HAFLA KULISAIDIA KUFANIKISHA ZIARA YA WAZIRI MKUU HAPA IRELAND.
KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YETU (WATANZANIA IRELAND), ZIARA YA WAZIRI MKUU ILITUPATIA FURSA YA KUJUMUIKA PAMOJA NA KUJISIKIA KUWA 'BADO TUNATAMBULIKA NA TAIFA LETU'. TUNATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI KWA MH. BALOZI MAAJAR NA TIMU YAKE KWA KUSHIRIKIANA NASI KAMA FAMILIA MOJA. WATANZANIA IRELAND MMEJIJENGEA SIFA NZURI. TUNAOMBA SISIMKO NA CHACHANDU ZA WIKI ILIYOPITA ZIWE CHANZO CHA KUIMARISHA UMOJA WETU.

ASANTENI

Sunday, March 1, 2009

Ziara ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda - Dublin Institute of Technology

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akikaribishwa na mwenyeji wake Prof. Brian Norton, President wa Dublin Institute of Technology, katika ziara yake katika chuo hicho tarehe 27/02/2009.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Msola wakiwa na wenyeji wao wa Dublin Institute of Technology. Kulia kutoka kwa Waziri Mkuu ni Prof. Brian Norton, President wa DIT, Dr. Fredrick Mtenzi mhadhiri wa DIT, na Prof. Godwin Mjema, mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha Tanzania, IFM.



Baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Dublin Institute of Technology-Ireland, wakiongea na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, tarehe 27/02/2009, alipokuwa kwenye ziara yake nchini  Ireland. 

Baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Dublin Institute of Technology, wakibadirishana mawazo kabla ya kumpokea Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, tarehe 27/02/2009, ikiwa ni moja ya ziara yake nchini Ireland.

HABARI KATIKA PICHA- Waziri Mkuu akiwa Dublin (Ireland)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakitembelea Kituo cha Mafunzo na Utafiti na Usindikaji Vyakula kilichopo Ashtown (Ashtown Food Research Centre) nje kidogo ya jiji la Dublin nchini Ireland akiwa katika ziara nchini Ireland Februari 27,2009


Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea zawadi ya maua kutoka kwa Katibu wa Umoja wa Watanzania waishio, Ireland, Bwana Makunja Jogoo wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipozungumza na watanzania hao jijini Dublin akiwa katika ziara ya kikazi nchini Ireland, Februari 27, 2008.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HABARI KATIKA PICHA- Waziri Mkuu akiwa Ireland (Ziara, DFA, Dublin)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe, Tunu (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pmoja na baadhi ya watanzania wanaoishi nchini Ireland katika hafla aliyoandaliwa Waziri Mkuu, Na Waziri wa Nchi wa Ireland, Peter Power, jijini Dublin Februari 25, 2009.



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Rais wa Ireland, Mary McAleese kwenye Ikulu ya nchi jijini Dublin kabla ya mazungumzo yao Februari 25, 2009. Alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Ireland.


Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati) na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani (kushoto) wkaiwa na baadhi ya watanzania wanaoishi nchini Ireland katika hafla aliyoandaliwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi wa Ireland, Peter Power jijini Dublin Februari 25 2009.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



HABARI KATIKA PICHA- Waziri Mkuu akiwa Ireland (Ziara,UCD)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozwa na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Dublin (UCD), Dr. Padraic onway na Profesa James Phelan ambaye ni Dean, Faculty of Agriculture, University College of Dublin wakati alipokwenda kwenye chuo hicho nchini Ireland Februari 26, 2009, kuwahutubia wahadhiLi na wanachuo akiwa katika ziara nchini humo.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali ya wahadhili na wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dublin nchini Ireland (UCD) baada ya kuwahutubia wakiwa katika ziara ya nchini humo Febraei 26,2009. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Dublin (UCD), Dr. Padrai Conway na kulia niProfesa James Phelan ambaye ni Dean, Faculty of Agriculture, University College of Dublin.(picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhio ya watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Dublin (UCD) nchini Irelanda baada ya kuwasili Chuoni hapo kuwahutubia wahadhili na wanachuo akiwa katika ziara nchini humo Februari 26,2009.(Picha na Ofisi ya Waziri MKuu)