Friday, February 27, 2009

UTARATIBU KUHUSU TAFRIJA, LEO JIONI 27.02.09

NDUGU WATANZANIA
SOTE TWAJUA UMUHIMU WA UGENI WA LEO JIONI. TUNAPENDA KUTANGULIZA HESHIMA NA ADABU WAKATI WA TAFRIJA KWA WAGENI WETU NA KWETU PIA. HIVYO BASI TUNAOMBA UTARATIBU UFUATAO UZINGATIWE:
  • Ni matumaini yetu kuwa majina yote yaliyotumwa kwa waandaaji kwa ajiri ya kuhudhuria tafrija leo, yalipokelewa na kuongezwa kwenye list. Majina hayo yalitumwa moja kwa moja kwa waandaaji na mengine kupitia kwa Watanzania Wenyeji hapa Ireland. "Iwapo hukutuma jina lako kuhusu kudhuria tafrija hii (lakini unayohabari ya tafrija hii na ukaamua kuhudhuria) hutaruhusiwa kuingia kwenye bwalo la chakula". Hii ni kwa sababu majina yote yamepelekwa kwa maafisa wa usalama; vilevile majina hayo yamekwisha pangiwa meza (Table Plan) hotelini
  • Kama unamjua mtu ambaye hakuleta jina lake na anampango wa kuja kesho tafadhali mwambie asihudhurie.
  • Ukishatambua meza yako waweza kubadilisha nafasi na kuhamia meza unayoipenda kwa kubadilishana na mtu wa meza hiyo.
  • Kopi za utaratibu wa tafrija zitatolewa kwa kila meza (TBC)
Asanteni
Waandaaji

No comments:

Post a Comment