Wednesday, February 18, 2009

Tangazo la kupotea kwa Passport ya Kitanzania

Habari za kazi Watanzania wenzangu muishio Ireland. Mimi ni mwanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania waliyopo Ireland. Hivi karibuni nimepoteza passport yangu maeneo ya Dublin 8. Nimeshaanza taratibu za kuomba passport nyingine kutoka ubalozini London. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mahitaji mengi yanayohitajika na ubalozi nimeshakamilisha. Ila bado sijafanikiwa kutangaza kwenye gazeti kuhusu kupotea kwa passport hio.

Hivyo basi, kufuatia maelezo haya naomba mwanajumuiya yeyote mwenye kufanya kazi au kufahamiana na jamaa yeyote mwenye kufanya kazi katika gazeti lolote la Ireland anisaidie hili. Naomba kuzingatia suala la bei, kwani kuna gazeti moja nilijaribu kuulizia nikaambiwa ni euro 200. Ikiwa ni gazeti la bure itakua vyema zaidi.

3 comments:

  1. Pole sana ndugu yangu. Hio kweli ni ngumu sana kwani tupo ugenini huku. Na inakua ngumu zaidi kwa mtu ambae ni mgeni kabisa.

    Mimi ushauri wangu ni kuwaomba viongozi wa jumuiya kuongea na ubalozi kuhusu kulegezwa kwa kigezo hicho kwa wanajumuiya. Kwani kama umeshapata maelezo kutoka polisi basi nadhani inatosha kabisa.

    ReplyDelete
  2. unaonaje ukajaribu local newspapers kuweka tangazo hilo kwa mfano gaziti la Northside People (linapatiikana free at your local supermaket)wanatoa tangazo kuanzia E25 kwa wiki

    ReplyDelete
  3. Jaribu Namba hii (1890-516-516) Herald AM, nimeongea nao wanachaji €39 kwa siku tatu mfululizo. The Irish Independent wanachaji €66 kwa Lost & Found.
    Mdau

    ReplyDelete