Utaratibu wa hafla ya Watanzania Ireland na Waziri Mkuu wa Jamh. ya Muungano wa Tanzania ni kama ifuatavyo:
- Ukumbi : Radisson SAS St. Helens Hotel, Stillorgan Dublin 4.
- Siku/Muda : Ijumaa, tarehe 27/02/09 Saa 2000 (saa mbili usiku)
- Usafiri : Basi litaondoka Great Denmark Street saa 1845 (saa kumi na mbili na dk45.) Denmark Street (tokea O'Connell St. kwa kutembea ni dk6) endelea mbele mpaka utakapouona mnara mrefu juu ya kanisa (kata kulia- umefika Grt Denamark street)
- Kama unatemegemea kwenda kwa usafiri wako tafadhali tuma baruapepe:swahili@live.ie;
- Iwapo jina lako lipo kwenye list na hatukupata taarifa toka kwako kuhusu kusafiri (kwa basi kwenda Radisson) tutachulia kwamba utakwenda kwa usafiri wako.
- Baada ya shughuli zote kumalizika basi litawarudisha watu mjini (muda saa tano usiku)
- Wageni wote mtatakiwa kuingia kwenye bwalo la chakula kabla ya kuwasili kwa Waziri Mkuu (mtatambulishwa kwa kengele)
- Kutakuwepo nafasi ya kumuuliza maswali matano Waziri Mkuu. Maswali yote yatapelekwa kwa Balozi, 25/02/09; siku ya hafla (kabla ya kuuliza swali) mwenyekiti atataja jina lako na utasimama na kuuliza swali lako. Utaratibu huu waweza kubadilika.
- Kama unaswali na unategemea kumuuliza Waziri Mkuu tafadhali litume: swahili@live.ie
- Kutakuwepo na utaratibu wa kupiga picha na Waziri Mkuu pamoja na wageni wengine kutoka Tanzania (mwishoni mwa shughuli zote). Tafadhali zingatia utaratibu utakaotolewa
Feel free to use either language, but we encourage lugha ya Taifa, Kiswahili.
Tafadhali vaa vazi la heshima na uwe nadhifu.
View Larger Map
Mimi naomba kuuliza je ni basi gani linapita huko, au kituo gani cha dart kiko karibu na hapo
ReplyDeleteanon hapo juu, basi ni namba 46A(best route in dublin), 63, 84, 58X.
ReplyDeleteDart kituo ni Booterstown, halafu unavuka barabara kwenye mataa, unafuata njia hiyo moja kwa moja mpaka utakapo kutana na barabara kubwa (N11) Trafic light set 3 toka stesheni, ukifika ya tatu unapinda kulia, halafu kulia tena kwenye mataa, ni muda wa dakika 10- 15 hivi.
Mimi naomba kuuliza je ni basi gani linapita huko, au kituo gani cha dart kiko karibu na hapo
ReplyDelete