Friday, February 27, 2009

UTARATIBU KUHUSU TAFRIJA, LEO JIONI 27.02.09

NDUGU WATANZANIA
SOTE TWAJUA UMUHIMU WA UGENI WA LEO JIONI. TUNAPENDA KUTANGULIZA HESHIMA NA ADABU WAKATI WA TAFRIJA KWA WAGENI WETU NA KWETU PIA. HIVYO BASI TUNAOMBA UTARATIBU UFUATAO UZINGATIWE:
  • Ni matumaini yetu kuwa majina yote yaliyotumwa kwa waandaaji kwa ajiri ya kuhudhuria tafrija leo, yalipokelewa na kuongezwa kwenye list. Majina hayo yalitumwa moja kwa moja kwa waandaaji na mengine kupitia kwa Watanzania Wenyeji hapa Ireland. "Iwapo hukutuma jina lako kuhusu kudhuria tafrija hii (lakini unayohabari ya tafrija hii na ukaamua kuhudhuria) hutaruhusiwa kuingia kwenye bwalo la chakula". Hii ni kwa sababu majina yote yamepelekwa kwa maafisa wa usalama; vilevile majina hayo yamekwisha pangiwa meza (Table Plan) hotelini
  • Kama unamjua mtu ambaye hakuleta jina lake na anampango wa kuja kesho tafadhali mwambie asihudhurie.
  • Ukishatambua meza yako waweza kubadilisha nafasi na kuhamia meza unayoipenda kwa kubadilishana na mtu wa meza hiyo.
  • Kopi za utaratibu wa tafrija zitatolewa kwa kila meza (TBC)
Asanteni
Waandaaji

Thursday, February 26, 2009

HABARI KATIKA PICHA 25.02.09


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akilisikiza hotuba ya Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ireland, Mr. Peter Power

Habari katika Video:PM Kwenye Makaribisho Ireland 25.02.09

Wednesday, February 25, 2009

Kukumbushana DFA Reception 25.02.09

Tunakumbushia kuwa 'Reception' ya leo jioni,DFA, itakuwa na ulinzi mkali; na admission ni kwa wale tu wenye 'Invitation Cards'. Watoto na Watu wasio na invitation Cards hawataruhusiwa kuingia. Hii ni 'Formal Gathering'(Tuheshimu utaratibu uliopangwa na DFA).Tafrija ya 27.02.09 pia yaweza kuwa na masharti haya, tunasubiri uamuzi wa Walinzi kuhusu watoto kutohudhuria.

Monday, February 23, 2009

TAFRIJA TAREHE 27.02.09 TANZANIA IRELAND DINNER WITH PRIME MINISTER

Ndugu Watanzania

Utaratibu wa hafla ya Watanzania Ireland na Waziri Mkuu wa Jamh. ya Muungano wa Tanzania ni kama ifuatavyo:
  • Ukumbi : Radisson SAS St. Helens Hotel, Stillorgan Dublin 4.
  • Siku/Muda : Ijumaa, tarehe 27/02/09 Saa 2000 (saa mbili usiku)
  • Usafiri : Basi litaondoka Great Denmark Street saa 1845 (saa kumi na mbili na dk45.) Denmark Street (tokea O'Connell St. kwa kutembea ni dk6) endelea mbele mpaka utakapouona mnara mrefu juu ya kanisa (kata kulia- umefika Grt Denamark street)
  • Kama unatemegemea kwenda kwa usafiri wako tafadhali tuma baruapepe:swahili@live.ie;
  • Iwapo jina lako lipo kwenye list na hatukupata taarifa toka kwako kuhusu kusafiri (kwa basi kwenda Radisson) tutachulia kwamba utakwenda kwa usafiri wako.
  • Baada ya shughuli zote kumalizika basi litawarudisha watu mjini (muda saa tano usiku)
Kwa kushauriana na maafisa wahusika toka ubalozini na Tanzania, yafuatatyo lazima kuzingatiwa:
  • Wageni wote mtatakiwa kuingia kwenye bwalo la chakula kabla ya kuwasili kwa Waziri Mkuu (mtatambulishwa kwa kengele)
  • Kutakuwepo nafasi ya kumuuliza maswali matano Waziri Mkuu. Maswali yote yatapelekwa kwa Balozi, 25/02/09; siku ya hafla (kabla ya kuuliza swali) mwenyekiti atataja jina lako na utasimama na kuuliza swali lako. Utaratibu huu waweza kubadilika.
  • Kama unaswali na unategemea kumuuliza Waziri Mkuu tafadhali litume: swahili@live.ie
  • Kutakuwepo na utaratibu wa kupiga picha na Waziri Mkuu pamoja na wageni wengine kutoka Tanzania (mwishoni mwa shughuli zote). Tafadhali zingatia utaratibu utakaotolewa
Nyongeza
Feel free to use either language, but we encourage lugha ya Taifa, Kiswahili.
Tafadhali vaa vazi la heshima na uwe nadhifu.


View Larger Map

Sunday, February 22, 2009

KUHUSU MAOMBI YA PASSPORT

Ndugu watanzania wenye kuhitaji kutengenezewa Passport- Afisa Uhamiaji atashughulikia maombi yanu tarehe 27.02.2009; Maldron Hotel, Parnell Square, D.1 Kuanzia saa Tatu na nusu asubuhi hadi saa sita mchana.

Rep. Tanzania Ireland

Thursday, February 19, 2009

Invitation by Department of Foreign Affairs.

Dear Tanzanians

The Department of Foreign Affairs would like to extend invitations to members of the Tanzanian community in Ireland to a reception in Iveagh House (Department of Foreign Affairs, 80 Stephen's Green Dublin 2) on Wed. 25th Feb.09 at 18:00PM.

Tunachukua Nafasi hii kuwafikishieni ujumbe wa mwaliko toka Wizara ya Mambo ya Nje ya Ireland, DFA. DFA inawakaribisheni nyote, wenye majina hayo hapo chini, kwenye party ndogo itakayofanyika Iveagh House (Department of Foreign Affairs, 80 Stephen's Green Dublin 2) Jumatano. 25th Feb.09.

Nyote mnaombwa kuhudhuria kwani mwaliko huu ni moja wapo ya shughuli za mapokezi ya waziri mkuu (Mizengo Pinda) hapo tarehe 26/02/09. Mwaliko huu ni tofauti na ule unaoandaliwa na ubalozi.

  1. Davina Mhando
  2. Fred Mtenzi
  3. David Nyauke
  4. Nam Kibacha
  5. Maria Mnzava
  6. Bebi Licky
  7. Maura Kachirode
  8. Zanifa Omary
  9. Dennis Lupiana
  10. James kasper
  11. Rukia Senga
  12. Rose Tinabo
  13. Msury Mahunnah
  14. Renatus Mushi
  15. Salehe Mwachaka
  16. Theresia Buluda
  17. Dickson Pinswande
  18. Alfred Mulla
  19. Zawadi Karashani
  20. Bw. Msafiri
  21. Bibi Msafiri
  22. Fredrik AJ Mashingia
  23. Luka Mkonongwa
  24. Frank Steven
  25. Eudoxia
  26. Amina Kavira
  27. Caroline Lamba
  28. Isabella Noone
  29. Thomas Kitambi
  30. Nakundwa Seushi
  31. Rukia
  32. Valentine Tungura
  33. Eudoxia Vitalis
  34. Bossi Masamilla
  35. Zubeir
  36. Marietha Mrema
  37. Nyamwenda Massamba
  38. Cecillia Massawe
  39. Salehe Mwachaka
  40. Jafari saidi
  41. Mwajuma Magwiza
  42. Baltazari Sungi

Shukrani
Wawakilishi: Tanzania Ireland

Tangazo la kupotea kwa Passport ya Kitanzania

Nitakua ni mbinafsi nisipotoa shukrani zangu za dhati kwa wanajumuiya wote mliotoa michango yenu kuhusiana na maada hii.

Nawashukuru sana, tena sana, kwani michango yenu imekua ni ya manufaa makubwa katika kuhitimisha zoezi la kutangaza kwenye gazeti kupotea kwa passport.

TWIGA ABATIZWA "NEEMA" DUBLIN ZOO


Wednesday, February 18, 2009

Tangazo la kupotea kwa Passport ya Kitanzania

Habari za kazi Watanzania wenzangu muishio Ireland. Mimi ni mwanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania waliyopo Ireland. Hivi karibuni nimepoteza passport yangu maeneo ya Dublin 8. Nimeshaanza taratibu za kuomba passport nyingine kutoka ubalozini London. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mahitaji mengi yanayohitajika na ubalozi nimeshakamilisha. Ila bado sijafanikiwa kutangaza kwenye gazeti kuhusu kupotea kwa passport hio.

Hivyo basi, kufuatia maelezo haya naomba mwanajumuiya yeyote mwenye kufanya kazi au kufahamiana na jamaa yeyote mwenye kufanya kazi katika gazeti lolote la Ireland anisaidie hili. Naomba kuzingatia suala la bei, kwani kuna gazeti moja nilijaribu kuulizia nikaambiwa ni euro 200. Ikiwa ni gazeti la bure itakua vyema zaidi.

Tuesday, February 17, 2009

JE UMEWEKA NAMBA 'ICE' KATIKA SIMU YAKO?

WEWE MTANZANIA UNAYEISHI MBALI NA NCHI YAKO, NDUGU, MARAFIKI AU WAPENDWA WAKO; JE UMEANDIKA NAMBA YA SIMU ''IN CASE OF EMERGENCY'' KWA KIFUPI, "ICE" KWENYE SIMU YAKO? Katika simu yako ya mkononi andika namba ya simu ya mtu ambaye atapigiwa simu wakati wa emergency- YOU NEVER KNOW!

Monday, February 16, 2009

Majadiliano ya mkutano 15/02/09

Kufuatia mkutano uliofanyika 15/02/09 yafuatayo ni baadhi ya mambo yaliyoongelewa.
  • Ada kwa mwaka kwa kila mwanaumoja wa Tanzania Ireland
  • mkakati wa kuiharisha chama- Katiba; account ya chama
  • Party ya watanzania- in the summer 09
  • Maandalizi ya kuonana na Waziri mkuu
Kwa maelezo zaidi kuhusu vidokezo hivyo hapo juu tuma barua pepe: swahili@live.ie

KUHUSU MAOMBI YA PASSPORT

Yah. Wenye maombi ya wenye kuhitaji pass za kitanzania. Tarehe maalumu ya kuonana na afisa uhamiaji hapa Dublin ni 26.02.09 na 27.02.09. Muda kamili haujatolewa.

Sunday, February 15, 2009

HAFLA YA WATANZANIA NA WAZIRI MKUU 27/02/09

Wapendwa Watanzania, kufuatia maongezi na ubalozi kuhusu ziara ya Warizi Mkuu. Ubalozi unatoa mwaliko wa chakula cha jioni na Waziri Mkuu tarehe 27/02/09. Yafuatayo ni majina yaliyokwisha tumwa kwa wawakilishi wa watanzania Ireland. Iwapo hutapenda kuhudhuria au jina lako halipo katika orodha hii tuma baruapepe kwenda swahili@live.ie
  1. Davina Mhando
  2. Fred Mtenzi
  3. David Nyauke
  4. Nam Kibacha
  5. Maria Mnzava
  6. Bebi Licky
  7. Maura Kachirode
  8. Zanifa Omary
  9. Dennis Lupiana
  10. James kasper
  11. Rukia Senga
  12. Rose Tinabo
  13. Msury Mahunnah
  14. Renatus Mushi
  15. Salehe Mwachaka
  16. Theresia Buluda
  17. Dickson Pinswande
  18. Alfred Mulla
  19. Zawadi Karashani
  20. Msafiri Mlangwa
  21. Rose Mlangwa
  22. Fredrik AJ Mashingia
  23. Luka Mkonongwa
  24. Frank Steven
  25. Eudoxia
  26. Amina Kavira
  27. Caroline Lamba
  28. Isabella Noone
  29. Thomas Kitambi
  30. Nakundwa Seushi
  31. Rukia
  32. Valentine Tungura
  33. Eudoxia Vitalis
  34. Bossi Masamilla
  35. Zubeir
  36. Marietha Mrema
  37. Nyamwenda Massamba
  38. Cecillia Massawe
  39. Salehe Mwachaka
  40. Jafari saidi