Jamani maajabu haya, yaletwa na Recession!
Huko county Limerick kumetokea maajabu kufuatia mti uliokatwa na watu, na kuacha alama (mfano wa picha) kubwa kwenye shina la lake; alama ambayo kwa kuiangalia kwa muda mrefu yajionesha kama picha ya Bikira Maria.
Yasadikika kuwa watu wawili waliohusika katika ukataji wa mti huo-walizidiwa wakati wa ukataji-walielemewa na mti- mti ulionekana kuwaangukia. Baada ya kugundua picha ya Bikira Maria ikijionesha, mti huo ulibadili uelekeo wa mwanguko na kuangukia upande tofauti. Tukio hili limevutia watu wengi toka Dublin kwenda kuabudu. Padre wa Parokia, karibu na tukio hili ameonya kuwa hakuna ishara yoyote ya uponyaji hivyo watu waache kuabudu mti. Mpaka hivi sasa watu wanazidi kuongezeka na kutoa sara zao. Pia yasemekana kuwa wengi wao wenye magonjwa mbalimbali wemeponywa.
Baada ya kuongea na wenyeji wa hapa Ireland, yaonekana kuwa matukio kama haya siyo mageni- kama kisiwa kilichowahi kuwa na watu wengi wachamungu mambo yaya yamewahi kutokea huko county Carlo na Cork. Lakini ajabu kubwa ni kwamba matukio kama haya hutokea sana hapa Ireland wakati wa Recession. Wenyeji wanadai kuwa tukio kubwa la ki-ushuhuda kama hili lilitokea huko Cork miaka ya 80 (Wakati wa recession kali hapa Ireland)
WALIMU NI NGUZO YA MAENDELEO-MAJALIWA
-
*WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa walimu ni nguzo kuu ya maendeleo
ya taifa lolote hapa duniani kwani ndio wanaotoa rasilimaliwatu yenye elimu
am...
4 hours ago
No comments:
Post a Comment